Serikali yakana kuwahangaisha viongozi wa upinzani pwani

0
2023
Kamishna wa kaunti ya Mombasa Evance Achoki

Mombasa, KENYA: Serikali imepinga madai kuwa inawahangaisha baadhi ya viongozi wa upinzani hasa katika ukanda wa Pwani.

Kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa siku ya jumatano, kamishna wa kaunti hiyo Evans Achoki alisema jukumu la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi analindwa bila kubagua.

Kamishna Achoki vile vile alitaka kiongozi yeyoye anayehofia usalama wake kupiga ripoti kwa idara ya usalama badala ya kutoa matamshi yanayoweza kuleta mgawanyiko miongoni mwa wakenya.

Kauli ya Achoki inakuja siku chache tu baada ya gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, kudai aliwakataa walinzi aliopewa na serikali kwa hofu kuwa walitumwa kwa lengo fiche wala sio kumlinda.


Imeharirirwa na Joseph Jira

Comments

comments