Nairobi:KENYA:Tume ya uchaguzi na mipaka nchini Iebc inasema imesajili angalau wapiga kura elfu 2 katika kila kaunti, katika zoezi linalondelea la kusajili wapiga kura.
Mkurugenzi mkuu wa tume ya Iebc Ezra Chiloba, alisema idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na ile waliyotarajia kusajili kwa siku.
Chiloba alisema tume hiyo inaweza kusajili idadi inayotarajia endapo watasajili angalau watu elfu 200 kwa siku kote nchini.
Iebcinalenga kusajili watu wapatao milioni sita kote nchini katika zoezi hilo litakalomalizika tarehe 14 mwezi ujao wa Februari.
Uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika tarehe 8 mwezi agosti mwaka huu wa 2017.
Imehaririwa na Joseph Jira