Mfanyabiashara Ali Punjani akana kupigana hadharani na wana wa Akasha

0
1426

Mombasa, KENYA:Mfanyabiashara wa Mombasa ameshtakiwa katika mahakama ya Mombasa kwa madai ya kupigana hadharani.

Mfanyabiashara huyo Ali Punjani alidaiwa kutishiana kwa bunduki na wana watatu wa marehemu Ibrahim Akasha, na raia mmoja wa kigeni baada ya kutofautiana katika hotel moja eneo la Kisauni mjini humo usiku wa kuamkia mwaka mpya.

Ali alikana mashtaka na hakimu Francis Kyiambia akaagiza aachiliwe kwa dhamana ya shilingi elfu 20 pesa tasilimu.

Wana hao wa marehemu Akasha, Baktash Akasha, Ibrahim Akasha, Abbdulsalam Akasha na raia wa India  Vijagiri Goswami walifunguliwa mashtaka ijumaa iliyopita kabla kuachiliwa kwa dhamana ya shiligi elfu 20.

Kesi  hiyo itasikizwa tarehe tatu mwezi aprili.

Baktash ,  Ibrahim na  Vijagiri wanakabiliwa na mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya humu nchini pamoja na nchini Marekani.

Comments

comments