Polisi Mombasa yamkamata mshukiwa mkuu wa ulanguzi wa mihadarati

0
1494

Mombasa,KENYA:Idara ya polisi mjini Mombasa inasema imemkamata mshukiwa mkuu wa ulanguzi wa dawa za kulevya na kupata maelfu ya pesa zinazoshukiwa zinatokana na mauzo ya dawa hizo eneo la Likoni.

Mshukiwa alitambulika kama Mohamed Tenga na kulingana na polisi alikamatwa eneo la Approved karibu na kituo cha polisi cha Inuka, akiwa na misokoto kadhaa ya dawa za kulevya aina heroine pamoja na shilingi elfu 12.

Mkuu wa polisi wilayani Likoni Willy Simba alisema mshukiwa amekuwa katika orodha ya washukiwa wanaosakwa na maafisa wa usalama, kwa kuhusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Mshukiwa atafikishwa mahakamani kufunguliwa mashtaka.

Imehaririwa na Joseph Jira

Comments

comments