Wanafunzi wajiunga na kidato cha kwanza

0
1547

Wanafunzi wa kidato cha kwanza wanajiunga na shule za upili kuanzia leo(jumatatu).

Takriban wanafunzi laki 5 wanatazamiwa kupata nafasi katika shule za upili.

Jumla ya wanafunzi elfu 780,walifanya mtihani wa kcpe mwaka jana.

Hayo yakijiri muungano wa walimu KNUT unataka uchunguzi wa kina ufanywe kuhusu matokeo ya mitihani ya kidato cha 4 KCSE mwaka jana.

Hii ni baada ya idadi kubwa ya wanafunzi kuanguka mtihani huo.

Wanafunzi elfu 33 walipata alama ya E ambayo ndio ya chini zaidi.

Comments

comments