Hakuna maandamano wakati huu wa corona- Mutyambai

0
1109

Hakuna maandamano yanayoruhisiwa  wakati huu taifa linapambana na janga la corona.

Huo ni usemi wake  Inspector-Generali wa polisi  Hillary Mutyambai ambaye ameonya wananchi dhidi ya mikusanyiko.

Akijibu masuali ya wakenya katika twitter, Mutyambai amesema kila mkenya sharti atii maagizo ya wizara ya afya ya kujikinga na corona.

Hii inafuatia kutiwa mbaroni kwa wanaharakati kadhaa walioandamana kushtumu kashfa ya ufujaji wa fedha za kupambana na janga la corona.

Comments

comments