Kaunti ya Taita Taveta yawapiga msasa mawaziri

0
1210

Taita Taveta, KENYA: Gasper Kabaka  ambaye aliteuliwa na gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granron Samboja kuchukua nafasi ya waziri maji amehojiwa na bunge la kaunti hiyo.

Kabaka aliileza kamati ya bunge kwamba  atahakikisha kampuni ya usambazaji wa maji katika kaunti hiyo [TAVEVO] inawajibika.

Ameahidi  kukabiliana na changamoto zote za maji ili kufaidisha wamananchi iwapo atachaguliwa katika wadhifa huo.

Bunge hilo pia limempiga msasa aliyeteuliwa kwa nafasi ya nyumba barabara na miundo msingi Houghton Msagha.

Wawili hao waliteuliwa upya na gavana samboja baada ya wengine kutopitishwa na bunge hilo.

Comments

comments