Wakristo washerehekea krismasi

Wakristo washerehekea krismasi

by -
0 237

Mombasa,KENYA: Wakristo kote ulimwenguni hii leo wanasherehekea siku kuu ya krismasi.

Hapa Mombasa waumini wamejumuika kanisani kwa ibada ya kukumbuka ya kuzaliwa kwa mwokozi yesu kristo.

Aidha watu wamesafiri maeneo tofauti kujimuika na ndugu jamaa na marafiki kusherekea siku hii.

Hapa Mombasa rais Uhuru Kenyatta amehudhuria misa ya krismasi.

Katika hotuba yake baada ya ibada, rais Kenyatta amewakumbusha wakenya umuhimu wa kudumisha amani.

Hayo yakijiri watalii kutoka sehemu tofauti wametembea fuo za bahari na mahoteli kujivinjari.

Usalama pia umeimarishwa huku maafisa wa polisi wakionekana wakishika doria sehemu kadhaa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES