Uzinduzi wa ferry ya Mtongwe wakwama

Uzinduzi wa ferry ya Mtongwe wakwama

by -
0 327

Mombasa,KENYA:Wakazi wa Mtongwe watasubiri zaidi kwa huduma za ferry kurudishwa eneo hilo.

Hii ni baada ya shirika la Kenya ferry kutangaza kuahirisha uzinduzi wa huduma hizo zilizotarajiwa kabla ya mwezi huu wa disemba.

Taarifa  iliyotiwa saini na mkurugenzi wa shirika hilo Bakari Gowa haijaeleza sababu za kuahirisha huduma za ferry ya Mtongwe.

Wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakitaka huduma hizo zirejelewe wakilalamikia msongamano mkubwa katika kivukio cha Likoni.

Comments

comments