Serikali yaanza kukagua wakimbizi kambini Daadab

Serikali yaanza kukagua wakimbizi kambini Daadab

by -
0 274
Kambi ya wakimbizi ya Daadab(Picha kwa Hisani)

Daadab,KENYA:Serikali imeanza zoezi la kukagua wakimbizi walio katika kambi ya Daadab, ili kuondoa wakimbizi gushi walio kambini humo.

Waziri wa usalama wa ndani Joseph Nkaissery alisema baadhi ya wakimbizi wamejiandikisha mara mbili na anataka watambuliwe katika zoezi hilo linalotarajiwa kuendelea hadi tarehe 31 mwezi huu.

Tayari baadhi ya wakimbizi wanaendelea kurejea nchini Somalia ikiwa ni katika harakati za Kenya kuifunga kambi hiyo ambayo ni kubwa zaidi duniani.

Serikali ilitangaza mpango wa kuifunga kambi hiyo ya Daabad kutokana na sababu za kiusalama.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES