Watu wanaoishi mpakani Taveta kupewa vitambulisho

Watu wanaoishi mpakani Taveta kupewa vitambulisho

by -
0 292

Taita Taveta, KENYA:Maelfu ya wakaazi wanaoishi eneo la mpakani huko Taita Taveta na wasio na vitambulisha vya kitaifa, wanatarajiwa kusajiliwa ili kupewa stakabadhi hiyo.

Hata hivyo kamishna wa kaunti ya Taita Taveta Kula Hache alisema wakaazi hao watakaguliwa kubaini waliongia nchini bila vibali na raia wa humu nchini, kabla ya vitambulisho hivyo kutolewa.

Wakazi hao wamekuwa wakilalamika kuhangaishwa na maafisa wa polisi kwa kukosa vitambulisho.

Aidha wanawake wanaotoka nchi jirani ya Tanzania walioolewa Kenya wamekuwa wakiitaka serikali iwape uraia ili wapate vitambulisho.

Wanasema inakuwa vigumu kwao kufanya kazi au biashara eneo la Taveta kwa kukosa vitambulisho.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES