Mtu ajiua kwa kujirusha majini kutoka kwa ferry Likoni

Mtu ajiua kwa kujirusha majini kutoka kwa ferry Likoni

by -
0 447

Mombasa,KENYA: Mwanamume mmoja amejitoa uhai kwa kujirusha baharini katika kivuko cha likoni hapa Mombasa.

Walioshuhudia wanasema mwanamume huyo alijirusha sehemu ya juu ya feri iliyokuwa ikivukisha abiria kutoka Likoni kuelekea upande wa kisiwani jumatatu.

Waokoaji wa baharini walipiga mbizi na kumtoa majini kabla ya maafisa wa shirika la msalaba mwekundu kujaribu kumfanyia huduma ya kwanza bila mafanikio.

Hayo yanakuja siku mbili tu baada ya mwanamke mmoja kujirusha baharini kutoka kwa Ferry kabla ya kuokolewa na waokoaji wa kivukio hicho.

Mwanamke huyo aliyetambuwa kwa jina Hadijah Abdullah atafikishwa mahakamani jumanne kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kujitoa uhai.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES