Wagonjwa wasusia huduma katika hospitali za Lamu

Wagonjwa wasusia huduma katika hospitali za Lamu

by -
0 367

Lamu,KENYA: Huku mgomo wa kitaifa wa madaktari na wauguzi ukiingia siku 3 leo, maafa yameripotiwa katika hospitali ya Coast General.

Hapo jumanne watu watatu waliripotiwa kuaga dunia kwa kukosa matibabu.

Lakini huko Lamu, wagonjwa wamedaiwa kugomea hospitali.

Inasemekana wauguzi walipigwa na butwaa baada ya wananchi kutofika kwa huduma licha ya kuwa wao hawakugoma.

Madaktari na wauguzi katika hospitali kuu ya kaunti (King Fahad) iliyoko mjini Lamu wanasema hamna mgonjwa ata mmoja aliyekuja kwa matibabu.

Baadhi ya wakaazi waliozungumza na Baraka FM wanadai kuwa wagonjwa wanaogopa kupitia mateso jinsi wanavyoshuhudia katika hospitali zingine za nchi ambapo kuna mgomo.

Huko Taita Taveta, serikali ya kaunti hiyo inasema itagharamia matibabu ya wagonjwa wa dharura na kina mama wanaojifungua katika hospitali za kibinafsi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES