Kenya ferry yaahirisha uzinduzi wa huduma za “Mtongwe ferry”

Kenya ferry yaahirisha uzinduzi wa huduma za “Mtongwe ferry”

by -
0 816
PHOTO FILE

Mombasa, KENYA: Shirika la Kenya Ferry limeahirisha uzinduzi wa huduma zake katika kivuko cha Mtongwe uliopaswa kufanyika Ijumaa tarehe 2 Disemba 2016.

Baraka Fm imebaini kwamba uzinduzi huo umeahirishwa kwa kuwa katibu katika wizara ya uchukuzi Irungu Nyakera, aliyetarajiwa kuongoza shughuli hiyo hangeweza kuhudhuria.

Afisa wa uhusiano mwema wa Kenya Ferry ameambia Baraka Fm kuwa tayari wamekarabati Ferry ya MV Harambee ambayo itatumika katika kivukio hicho huku wakiendelea kukarabati nyingine ya MV Nyayo.

Kwa mujibu wa Kenya Ferry, ferry ya Mtongwe inaweza kuvukisha hadi abiria elfu 13 kwa siku na kupunguza msongamano wa abiria na magari katika kivukio cha Likoni.

Abiria wapatao  wapatao elfu 300 hutumia kivukio vha Likoni kila siku.

Huduma za usafiri katika kivuko cha Mtongwe zilisitishwa miaka 22 iliyopita, kufuatia mkasa wa ferry ya MV Mtongwe iliyozama mwaka 1994 ambapo takriban watu 270 walipoteza maisha.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES