Wanafunzi wa Agha Khan wafaulu KCPE huku rais akimsifu Matiang’i

Wanafunzi wa Agha Khan wafaulu KCPE huku rais akimsifu Matiang’i

by -
0 483
Muhammad Hassan Awadhan kushoto) na Zainab Zeinuddin wote wawili kutoka shule ya msingi ya Agha Khan Academy Mombasa. PHOTO:COURTESY

Mombasa,KENYA:Shangwe na nderemo zilitanda katika shule ya msingi ya Agha Khan hapa Mombasa, baada ya wanafunzi wawili kuwa miongoni mwa wanafunzi bora katika mtihani wa kitaifa wa darasa la nane wa KCPE mwaka huu wa 2016.

Zainab Zeinuddin na Muhammad Hassan Awadhan wote wa shule ya Aga Khan walipata alama 415 na 422 mtawalia.

Mwanafunzi bora wa mtihani huo wa KCPE mwaka huu ni Victor Odhiambo kutoka shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ya Daisy huko Kakamega amepata alama 439 kati ya 500.

Akitangaza matokeo hayo, waziri wa elimu Fred Matiangi alisema alama hiyo imepungua ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Aidha aliarifu kuwa hakuna mwanafunzi yeyote atayekosa matokeo yake ya KCPE mwaka huu.

Alieleza kuwa shughuli ya  uteuzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza  itaanza rasmi tarehe 9 mwezi huu na wanafunzi hao kuripoti shule za upili tarehe 9  januari.

Wakati huo huo Rais Uhuru Kenyatta amemsifu waziri huyo kwa utendakazi wake hasa kuhakikisha KCPE inafanyika bila visa vya udanganyifu.

Rais Kenyatta pia amemtaka waziri Matiang’i kuendelea na mfumo wa mageuzi katika idara ya elimu nchini ili kuhakikisha mtihani huo unakuwa wa kuaminika.

Comments

comments