Mahakama kuamua iwapo interpol ihusishwe kwa kesi ya kifo cha Muingereza

Mahakama kuamua iwapo interpol ihusishwe kwa kesi ya kifo cha Muingereza

by -
0 245

Mombasa,KENYA: Mahakama ya Mombasa Alhamisi tarehe  30 Novemba, inatarajiwa kutoa uamuzi iwapo polisi wa kimataifa-Interpol kutoka Uingereza watahusishwa  katika kesi ya kifo cha kutatanisha cha raia wa Uingeraza hapa Mombasa mwaka 2013.

Marehemu Harry Veevers alifariki katika hali ya kutatanisha nyumbani kwake Nyali na baadaye mahakama ikaagiza  mwili wake ufukuliwa mwaka wa 2014 kwa uchunguzi wa kiini cha kifo chake.

Hii ni baada ya Richard Veevus-mwanawe marehemu kuelekea mahakamani kutaka kufahamu chanzo cha kifo cha babake akidai mama yake wa kambo Azra Parveen Din na ndugu wake wa kambo Alexandar Veevers na Hellen Veevers walihusika kwa mauji ya  babake.

Mwanae marehemu pia anataka daktari kutoka humu nchini aliyekuwa akitibu  babake, kufika kortini na kuelezea hali ya afya ya marehemu alipokuwa humu nchini.

Mwendesha mashtaka – Alexandar Muteti alipinga hatua ya polisi wa kimataifa kuhusishwa katika kesi hiyo  akisema kuwa polisi wa Kenya wana uwezo wa kufanya uchunguzi kupitia kwa ofisi ya mwendesha mashtaka nchini.

Hayo yakijiri tofauti zinazidi kujitokeza kortini  kati ya madaktari kuhusu kifo cha Veevers.

Comments

comments