Abdulswamad apeleka bungeni mswada wa kuwafidia polisi

Abdulswamad apeleka bungeni mswada wa kuwafidia polisi

by -
0 316
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharrif

Mombasa,KENYA: Mbunge wa Mvita Abdul Swamad Sharrif Nassir anasema aliwasilisha mswada bungeni kuhakikisha maafisa wa polisi wanapokea fidia kikamilifu haswa wanapouawa au kuumia wakiwa kazini.

Akizungumza na Baraka Fm  bungeni mjini Nairobi, Abdul Swamad alisema mswada huo utahakikisha kuwa inakua sheria kwa fidia hiyo kutolewa kwa maafisa wa polisi na familia yao wanapokumbwa na maafa  .

Alieleza kuwa  aliwasilisha mswada huo bungeni kwani maafisa wa polisi na familia zao huteseka kupata fidia hiyo pindi wanapokumbana na maafa au majeruhi wakiwa kazini.

Mswada huo tayari umesomwa kwa mara ya pili bungeni na unatarajiwa kupita awamu zingine kabla ya kupitishwa.

Baadae rais Uhuru Kenyatta ataitia sahihi kuwa sheria iwapo wabunge watauuidhinisha mswada huo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES