Serikali ya Mombasa yajitayarisha kukabili mafuriko

Serikali ya Mombasa yajitayarisha kukabili mafuriko

by -
0 410

Mombasa, KENYA: Serikali ya kaunti ya Mombasa inasema imejiandaa kudhibiti hali iwapo kutatokea mafuriko kufuatia mvua iliyoanza kunyesha hapa Mombasa.

Afisa wa mawasilino katika kaunti Richard Chacha aliambia Baraka FM kuwa kaunti tayari imebuni kitengo maalum kitakachotoa msaada wa dharura kwa wakazi.

Chacha vilevile alisema serikali ya kaunti kupitia wizara ya afya tayari imetoa dawa za kutibu maji ya kunywa ili kuzuia magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu.

Mvua kubwa inayonyesha nchini kwa sasa inahofiwa kuwa heunda ikasababisha mafuriko hasa katika sehemu za nyanda za chini.

Wakazi wanahimizwa kuchimba mitaro ya kupitisha maji au hata kuhamia sehemu zilizoinuka.

Hapa Mombasa baadhi ya barabara hazipitiki kutokana mafuriko, huku madereva wa magari wakilazimika kutafuta barabara salama. Katika mtaa wa Mikindani, mafuriko yamesababisha barabara hiyo kujaa maji.

Eneo lingine lisilopitika ni King’orani karibu na kituo cha railways kutokana na barabara hiyo ya mkato kujaa maji.

Mvua imeanza kushuhudiwa Mombasa na pwani kwa jumla baada ya kipindi kirefu cha msimu wa jua hali iliyosababisha ukame na uhaba wa chakula maeneo ya Ganze.

 

Taarifa zaidi na George Otieno

Comments

comments