Mkurugenzi wa shule akamatwa kwa kuzuia watahiniwa kufanya KCSE

Mkurugenzi wa shule akamatwa kwa kuzuia watahiniwa kufanya KCSE

by -
0 293

Likoni, KENYA: Polisi Likoni wamemkamata mkurugenzi wa shule ya upili ya Likoni Community kwa madai ya kuwazuia watahiniwa kufanya mtihani wa kitaifa wa shule za upili KCSE.

Mshukiwa huyo Obuya Otieno Ritzau amekamatwa na maafisa wa upelelezi baada ya wanafunzi hao kuonekana wakiwa nje wakati mtihani ukiendelea.

Polisi wanasema mshukiwa aliwazuia watahiniwa watatu kufanya mtihani huo wa somo la Bayologia kwa madai hawakuwa wamekamilisha kulipa karo.

Maafisa wa polisi waliokuwa wakilinda mtihani huo waliwaarifu wenzao ambao walifika na kumkamata mshukiwa.

Wanafunzi hao waliojawa na hasira waliandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Likoni.

Mkuu wa polisi Likoni Willy Simba anasema mshukiwa ameandikisha taarifa kwa polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES