Mahakama ya Mombasa sasa itaamua ikiwa wana wa marehemu Akasha watashtakiwa Marekani

Mahakama ya Mombasa sasa itaamua ikiwa wana wa marehemu Akasha watashtakiwa Marekani

by -
0 478
Wana wa Akasha kuanzia kushoto: Baktash Akasha, Vijaygiri Anandgiri, Gulam Hussein na Ibrahim Akasha wakiwa mahakamani Mombasa.

Mombasa, KENYA: Mahakama ya Mombasa sasa itasikiliza kesi na kutoa uamuzi iwapo wana wawili wa marehemu Ibrahim Akasha na wenzao wengine wawili, watasafirishwa hadi nchini Marekani kujibu tuhuma za ulanguzi wa dawa za kulevya.

Uamuzi huo una maana kuwa mahakama hiyo imekataa ombi la upande wa mashtaka la kutaka washukiwa hao wasafirishwe  moja kwa moja bila idhini yake.

Hakimu Julius Nang’ea amesema sheria baina ya Kenya na Marekani inaruhusu washukiwa hao kusikilizwa, kabla ya korti kutoa uamuzi.

Awali mahakama iliahirisha kutoa uamuzi baada ya washukiwa wengine kukosa kufika kortini ambapo wakili wao alisema walikuwa na matatizo ya kiafya.

Mahakama hata hivyo imewaonya dhidi ya kukwepa vikao vya korti bila sababu mwafaka ikisema huenda wakaadhibiwa kwa kutupilia mbali dhamana iliyowaachia huru na hivyo kuzuiliwa.

Wakati huo huo mahakama kuu ya Mombasa Ijumaa inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu kupunguza kiwango cha dhamana kwa washukiwa hao wanne.

Hii ni baada ya washukiwa hao kusema dhamana ya shilingi milioni 30 kila mmoja ni kubwa.

Baktash Akasha Abdalla, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha Abdalla na Vijaygiri Anandgiri Goswami wanahusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya heroine humu nchini na pia nchini Marekani.

Mhariri: Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES