Ruto asema bandari ya Mombasa haiuzwi wala kubinafsishwa

Ruto asema bandari ya Mombasa haiuzwi wala kubinafsishwa

by -
0 285

Mombasa,KENYA: Naibu rais William Ruto amekariri kuwa serikali haina mpango wa kubinafsisha bandari ya Mombasa.

Akiongea alipokutana na wafanyakazi wa bandari katika eneo la Mabaraki hapa Mombasa, Ruto alisema  habari zinazoenezwa kuhusu bandari hiyo hazina msingi wowote.

Naibu rais alisema haiwezekani serikali kutumia fedha nyingi kupanua bandari hiyo kisha kuibinafsisha.

Aidha ametangaza kwamba yeye pamoja na rais Uhuru Kenyatta watakutana na maakuli wa bandarini kusikia kilio chao kuhusu bandari.

“Tunataka kufanya mkutano na maakuli wa bandarini kable mwezi wa disemba ili tutatue shida zinazowakumbwa wafanyakazi wa bandari”, Ruto alisema.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES