Mahakama yatoa uamuzi kuhusu idadi ya wadi

Mahakama yatoa uamuzi kuhusu idadi ya wadi

by -
0 254

Mombasa, KENYA: Mahakama kuu ya Mombasa imetoa uamuzi wa kuondoa kipengee cha 26 cha sheria kuhusu serikali za kaunti kilichosema ni lazima kaunti iwe na angalau wadi 15.

Uamuzi huo unafuatia ombi lililowasilishwa katika mahakama hiyo na tume ya uchaguzi na mipaka  nchini IEBC  kutaka kipengee hicho kiondolewe.

Hayo yalijiri baada ya kaunti ya Lamu kushtaki tume hiyo kwa kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka 2013, bila kuzingatia kipengee hicho na sasa  jaji Emukule Anyara pia ametupilia mbali kesi hiyo.

Hapo awali wakili anayewakilisha kaunti ya Lamu Yusuf Abubakari, alisisitita kuwa kipengee hicho  kinalazimu kaunti kuwa na wadi 15 au zaidi kwa uchaguzi mkuu, lakini hilo halikuzingatiwa katika kaunti ya Lamu.

Wakaazi wa Lamu walilalamika kuwa kaunti hiyo ina wadi 10 pekee, na ililazimu IEBC kupeana nafasi nyingi za kuteua wawakilishi wa wadi ili kufikisha idadi inayohitajika, jambo walilosema lilikuwa ni kinyume na sheria.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES