Naibu gavana wa Kwale pia atimuliwa kutoka chama cha ODM

Naibu gavana wa Kwale pia atimuliwa kutoka chama cha ODM

by -
0 1159

Kwale, KENYA:Viongozi wa chama cha ODM kaunti ya Kwale wamemtimua naibu gavana wa kaunti hiyo Bi. Fatma Achani kwenye chama siku chache baada ya kumfurusha gavana Salim Mvurya.

Wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kwale ambaye ni mbunge wa Matuga Hassan mwanyoha, viongozi hao wamedai bi Achani hajakuwa mwaminifu kwa chama hicho.

Wakiwa pamoja na seneta wa eneo hilo Juma Boi Juma na spika wa bunge la Kwale Sammy Ruwa viongozi hao wamedai bi Achani amekuwa kibaraka wa chama cha Jubilee siku chache tu baada ya gavana Mvurya kuuhama muungano wa CORD na kujiunga na Jubilee.

Wakati huohuo wametoa onyo kwa maafisa wa serikali wanaodaiwa kupigia debe chama kipya cha jubilee katika kaunti hiyo ya kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES