Mwanafunzi wa Chuo kikuu ahusishwa na kundi la kigaidi la ISIS

Mwanafunzi wa Chuo kikuu ahusishwa na kundi la kigaidi la ISIS

by -
0 536
Hassan Kassim Hassan anayedaiwa kutaka kujiunga na kundi la kigaidi la ISIS.

Mombasa, KENYA: Mahakama ya Mombasa imeagiza polisi wamzuilie kwa siku 10 zaidi, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Moi, Eldoret anayedaiwa kuwa mwanachama wa kundi la  kigaidi la ISIS.

Uamuzi huo onafuatia ombi lililowasilishwa katika mahakama ya Mombasa na kiongozi wa mashtaka Eugene Wangila kutaka mwanafunzi huyo azuiliwe kwa muda zaidi ili polisi wakamilishe uchunguzi.

Wangila aliiomba mahakama imzuilie mshukiwa katika kituo cha polisi cha Nyali, Mombasa kwa siku 15.

Hassan Kassim Hassan alikamatwa Jumatatu eneo la Kizingo mjini Mombasa kufuatia taarifa za idara ya ujasusi.

Awali, Kiongozi wa mashtaka aliambia mahakama kuwa mawasiliano ya mshukiwa yalionesha  amekuwa akiwasiliana na wanachama wa kundi la kigaidi la ISIS na alikuwa anapanga kusafiri kuelekea nchini Libya ili kujiunga rasmi na kundi hilo la kigaidi.

Kwa muda sasa, idara ya usalama ya Kenya imekuwa ikikabiliana na makundi ya kigaidi hasa kundi la Alshabaab kutoka nchini Somalia.

Mhariri: Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES