Jaji mkuu akutana na Raila, Kalonzo na Wetangula

Jaji mkuu akutana na Raila, Kalonzo na Wetangula

by -
0 480
Viongozi wa upinzani wakikutana na jaji mkuu David Maraga ofisini mwake mjini Nairobi. PICHA: HISANI

Nairobi, KENYA: Jaji mkuu David Maraga amekutana na viongozi wa upinzani CORD waliomtembelea ofisini kwake mjini Nairobi.

Katika mkutano huo, jaji mkuu aliwahakikishia CORD kuwa mahakama itasikiliza kesi ya rufaa ya uchaguzi iwapo itawasilishwa.

Viongozi wa CORD waliokutana na Maraga ni pamoja na Raila Odinga, Moses Wetangula na Kalonzo Musyoka.

Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, jaji mkuu aliwataka wakenya kuendeleza Amani inayoshuhidiwa kwa sasa nchini.

Maraga aliapishwa rasmi mwezi jana wa Oktoba kuchukua nafasi ya Willy Mutunga aliyestaafu.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES