Mahakama yakataa kutupilia mbali kesi inayomkabili MCA wa eneo la Shanzu

Mahakama yakataa kutupilia mbali kesi inayomkabili MCA wa eneo la Shanzu

by -
0 324

Mombasa, KENYA: Mahakama ya Mombasa imetupilia mbali ombi lillilowasilishwa kortini na mfanyabiashara wa hapa Mombasa kutaka kesi ya ufisadi inayomkabili mwakilishi wa wadi ya Shanzu itupiliwe mbali.

Ombi hilo liliwasilishwa na mlalamishi katika kesi hiyo akisema angependa kesi itupiliwe mbali kwa kuwa amekuwa akitishiwa maisha tangu aiwasilishe kortini.

Maurine Aketch ambaye ni mlalamishi katika kesi hiyo aliambia  mahakama hapo awali kuwa amekuwa akipokea simu na jumbe fupi za kumtishia maisha na anahisi ni kutokana na kesi hiyo.

Lakini hakimu Teresia Matheka amesema washukiwa katika kesi hiyo wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na kutaka kesi hiyo iendelee kusikilizwa na kuamuliwa kama njia moja ya kupiga vita ufisadi nchini.

Matheka pia amekataa  ombi la kiongozi wa mashtaka la kutaka kesi hiyo iahirishwe na kusikizwa siku nyingine.

Mlalamishi ataka kesi dhidi ya MCA wa Shanzu iondolewe akidai kutishiwa maisha

Kiogozi wa mashtaka Eugine Wagila amesema atakata rufaa kufuatia uamuzi wa mahakama wa kukataa kuahirisha kesi hiyo.

Katika kesi hiyo, Mwakilishi wa wadi ya Shanzu iliyo kaunti ya Mombasa Maimuna Mwasasi pamoja na Christopher Karisa wanakabiliwa na shtaka la kupokea shilingi milioni moja unusu kutoka kwa Mourine Aketch kwa madai wangemsaidia kusuluhisha mzozo  wa shamba dhidi yake na serkali ya kaunti.

Mhariri: Eliakim Mwachoni

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES