Polisi yasaka washukiwa wa ujambazi wenye silaha hatari Mombasa

Polisi yasaka washukiwa wa ujambazi wenye silaha hatari Mombasa

by -
0 294

Mombasa,KENYA:Polisi eneo la Kisauni mjini Mombasa wanasema wanawasaka washukiwa wawili wa ujambazi waliojihami kwa silaha hatari ambao jaribio lao la kutaka kutekeleza wizi eneo hilo lilitibuka.

Washukiwa hao waliokuwa kwa pikipiki walisemekana kumvamia mwanamke mfanyabiashara aliyekuwa akipeleka pesa benki kabla ya kufumaniwa eneo la Naivas Nyali.

Polisi walisema washukiwa walitoroka kwa pikipiki baada ya mwanamke huyo kupiga kelele zilizovutia watu wengi.

Mkuu wa polisi kisauni Richard Ngatia alihimiza wafanyabiashara kuitisha msaada ya polisi wanapopeleka kiwango kikubwa cha pesa katika benki ili kuepuka visa kama hivyo

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES