Sherehe za mashujaa dei zakumbwa na vurugu Mombasa na Kilifi

Sherehe za mashujaa dei zakumbwa na vurugu Mombasa na Kilifi

by -
0 416

Mombasa, KENYA:Sherehe za mashujaa ziligeuka na kuwa vurugu kwa muda mjini Mombasa baada ya wafuasi wa vyama mbalimbali vya kisiasa kuzomeana.

Watu waliodaiwa kuwa wafuasi wa gavana wa Mombasa Hassan Joho walizozana wa wale wa mbunge wa Nyali Hezron Awiti pamoja na wale wa chama kipya cha Jubilee.

Vurugu hizo zilionekana kuchochewa na matamshi ya baadhi ya viongozi waliochukua fursa ya sherehe kupigia debe vyama vyao vya kisiasa.

Iliwabidi maafisa wa polisi waingilie kati na kutuliza hali, ambapo baadae viongozi waliendelea kuhutubia.

Huko Kilifi hafla hiyo ya mashujaa dei ilitatizwa kwa muda kufuatia fujo za wananchi waliokuwa wamebeba mabango yenye majina ya wanasiasa.

Inasemekana kamishna wa kaunti hiyo Joseph Keter alilazimika kupanda jukwaani kutuliza hali kabla ya sherehe kuendelea.

Wakati huo huo rais Uhuru Kenyatta amewataka wakenya kujiepusha na viongozi wanaohubiri siasa za chuki wakati uchaguzi mkuu ukanaribia.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya mashujaa, mjini Machakos, rais Kenyatta alisema wakenya wanafaa kufanya maamuzi ya busara na kuchagua viongozi waadilifu ambao wataleta maendeleo kwa wakenya.

Rais pia alisema wanashirikiana na serikali za kaunti kukabiliana na janga la njaa na ukame.

Wakati huo huo kiongozi wa taifa alisema wamewaachia huru wafungwa elfu saba waliokuwa wanakabiliwa na makosa madogo madogo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES