Malik Obama kualikwa na Donald trump katika mdhahalo wa Urais

Malik Obama kualikwa na Donald trump katika mdhahalo wa Urais

by -
0 504
Malik Obama (left) and US president Donald Trump

Mwaniaji urais na tikiti ya Republican nchini Marekani Donald Trump amemualika ndugu wa kambo wa Rais Barack Obama Malik Obama kuwa mgeni wake katika mdahalo wa urais utakao fanyika leo usiku katika mji wa Las vegas , Nevada.

Malik Obama ambaye ni mfuasi wa dini ya kiislamu na ana uraia wa Marekani na Kenya, anasema kuwa alikuwa mfuasi wa chama cha Democrat lakini akahamia chama cha Republican kutokana na kugadhabishwa na uongozi wa ndugu yake.

Katika mahojiana na gazeti ya Marekani ya New York Post Malik aliulaumu utendakazi wake Hillary Clinton alipokuwa katibu wa Marekani huku akimlaumu kuwa chanzo cha machafuko katika inchi nyingi za Asia ya kati na Kaskazini mwa Afrika ikiwemo Libya.

Kando na hayo Malik amemtetea Trump kutokana na madai ya ngono ambayo yamekuwa yakimkumba hivi karibuni huku akihoji uaminifu wa madai hayo.

Malik ambaye ni mkubwa wake Obama na miaka tatu aliwahi kuwania ugavana wa kaunti ya Siaya katika Uchaguzi wa mwaka 2013 .

Comments

comments