Maelfu ya wakazi wa Taita Taveta na Kwale pia wakumbwa na baa...

Maelfu ya wakazi wa Taita Taveta na Kwale pia wakumbwa na baa la njaa

by -
0 478

Kwale,KENYA: Zaidi ya wakaazi laki moja huko kaunti ya kwale wameripotiwa kuathirika na ukame.

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kinango, Ndavaya, Samburu ,Chengoni na Maknon road pamoja na Lunga lunga.

Mifugo  pia imeripotiwa kufariki kutokana na ukosefu wa lishe.

Roman Shera ambaye ni mshirikishi katika mamlaka simamizi ya maswala ya ukame kaunti ya kwale alisema huenda hali ikawa mbaya zaidi.

Wakati huo huo zaidi ya watu laki moja kutoka kaunti ya Taita Taveta nao wanakabiliwa na baa la njaa huku wazee na walemavu wakitajwa kuathirika zaidi.

Kamishena wa kaunti hiyo Josephine Onunga alitoa wito kwa wahisani kushirikiana na serikali katika harakati za kutoa misaada wa chakula kuwasaidia wahanga.

Eneo la Ganze hali imezidi kuwa mbaya huku mifugo wakifariki kutokana na ukosefu wa lishe na maji.

Hatua hiyo ililazimu serikali kutangaza kuwa itanunua mifugo waliodhoofika na kuwachinja ili kuwapa wananchi wa eneo hilo chakula.

Taarifa hii imeandikwa na Lawrence Sita (Kwale) na Fatuma Rashid (Taita Taveta)

Mhariri: George Otieno

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES