Afisa wa NIS akamatwa na kufungwa katika mlingoti wa stima Likoni

Afisa wa NIS akamatwa na kufungwa katika mlingoti wa stima Likoni

by -
0 370

Mombasa, KENYA: Kulizuka kizaa katika mtaa wa Ujamaa huko Likoni mjini Mombasa baada ya afisa mkuu wa polisi anayedai kuhudumu katika idara ya ujasusi-NIS, kukamatwa na maafisa wa upelelezi na kufungwa kwenye mlingoti wa stima kwa zaidi ya muda wa saa mbili.

Afisa huyo aliyetembulika kama Rajab Mwamchiri anayedaiwa kuhudumu eneo la Ngong jijini Nairobi alikamatwa karibu nyumbani kwake jumanne jioni alipokwenda kudai redio yake kwa fundi aliyekuwa akiirekebisha.

Afisa huyo aliambia baraka fm kuwa alipowasili katika kibanda cha fundi kuulizia radio yake, aliagizwa kusubiri kwa kuwa redio yake haikuwa tayari.

“Punde si punde nimesimama hapo nje,niliona gari nyeusi aina ya Subaru ambayo hutumiwa na maafisa wa cid likoni, nilifikiri walikuwa katika kazi zao za kawaida lakini nikashtuka nmekamatwa na kufungwa pingu mkononi bila hata maafisa hao kutamka lolote”, alisema afisa huyo.

Hatua hiyo ilisababisha umati wa watu kukusanyika.

Maafisa wengine wawili wa CID walitoroka wakiohofia kukabiliwa na umati huku mmoja aliyekuwa na bastola akiachwa pekee na afisa aliyekuwa amefungwa.

Inasemekana ilibidi maafisa wengine kutoka kituo cha polisi cha Inuka huko Likoni kuitwa ili kutuliza umati uloitaka kumteketeza afisa wa CID pamoja na gari lao, wakisema afisa wa NIS aliyekuwa amekamatwa hakuwa na hatia.

Rajab alidai alikuwa mwalimuwa madrassa kwa muda wa miaka 10 kabla kujiunga na idara ya NIS.

Alidai maafisa wa CID likoni wamekuwa na njama na fundi huyo wa redio kuibia watu mali yao.

Naibu mkuu wa polisi wilayani Likoni huko Mombasa Anthony shimoli alibitisha kisa cha afisa huyo kukamatwa, akisema fundi wa radio aliripoti kwa polisi kuwa afisa huo wa NIS alikuwa anawatishia maisha siye aliyepeleka radio kurekebishwa.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES