Watu 15 waugua baada ya kula mihogo yenye sumu huko Marafa

Watu 15 waugua baada ya kula mihogo yenye sumu huko Marafa

by -
0 429

Kilifi,KENYA:Jumla ya watu 15 kutoka kijiji cha Bore Singwaya huko Marafa – Magarini kaunti ya Kilifi wanaugua baada ya kula mihogo inayoshukiwa huenda ilikuwa na sumu kutokana na makali ya njaa.

Inadaiwa jamii ya eneo hilo ilichimba mihogo hiyo ambayo imekaa katika shamba kwa muda mrefu.

Dhahabu Katana Wanje ambaye ni mmoja wa walioathirika kwa kula mihogo hiyo, alisema kuwa watoto ndio walioathirika zaidi.

Daktari msimamizi wa hospitali ya Marafa George Angore alithibitisha kuwa idadi ya waathiriwa wengi ni watoto ambapo watoto kumi na wawili bado wanaendelea kupokea matibabu.

Wakati huo huo zaidi ya mifugo elfu moja wamefariki katika muda wa miezi mitatu huko Ganze kaunti ya Kilifi kufuatia ukame.

Mkaazi mmoja aliyezungumza na Baraka FM kwa jina Joseph Charo, alisema eneo liliathirika sana ni Goshi ambako mifugo wengi wameangamia.

Alisema kwa sasa wanategemea maji kutoka bwawa la Renji ambalo pia maji yake imepungua.

Wakazi walisema wanalazimika kutembea zaidi ya kilomita 30 kufikia bwawa hilo.

Taarifa zaidi imetumwa na David Ngumbao na kuhaririwa na George Otieno

Comments

comments