Kenya yataka wana wa Ibrahim Akasha kufunguliwa mashtaka nchini Marekani

Kenya yataka wana wa Ibrahim Akasha kufunguliwa mashtaka nchini Marekani

by -
0 574
Wana wawili wa marehemu Ibrahim Akasha(kushoto na kulia) wakiwa kizimbani.Kenya inataka wajibu mashtaka nchini Marekani. PICHA:MAKTABA

Mombasa,KENYA:Mkuu wa mashtaka ya umma hapa pwani Alexander Muteti anawataka wana wa mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati marehemu Ibrahim Akasha pamoja na washukiwa wengine wajisalimishe kwa vyombo vya kisheria vya Marekani ili kujibu kesi dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya.

Muteti ameambia mahakama kuwa kesi iliyowasilishwa kortini kupinga washukiwa hao kufunguliwa mashtaka nchini Marekani, ni njama ya kupoteza muda wa kesi hiyo kuendelea.

Baktash Akasha Abdalla, Gulam Hussein, Ibrahim Akasha Abdalla na Vijaygiri Anandgiri Goswami wanahusishwa na ulanguzi wa dawa za kulevya aina ya heroine.

Wakili wa washukiwa Pro. George Wajackoyah ameambia mahakama kuwa wateja wake walikamatwa humu nchini wala si Marekani, hivyo haikuwa haki kushtakiwa nchini Marekani.

Wajackoyah amesisitiza kuwa kuwasafirisha wateja wake nchini Marekani ni ukiukaji wa katiba ya taifa.

Muteti amesema katiba ya nchini pamoja na mikataba ya kisheria kati ya Kenya na Marekani inaruhusu washukiwa hao kufunguliwa mashtaka nchini humo.

Hakimu Douglas Ogoti amesema mahakama itatoa uamuzi Novemba 9.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES