Kidero apigiwa kura ya kumtoa uongozini

Kidero apigiwa kura ya kumtoa uongozini

by -
0 286

Nairobi,KENYA:Bunge la kaunti ya Nairobi jumanne lilipitisha hoja ya kujadili hatua ya kumng’oa mamlakani gavana Evans Kidero.

Wawakilishi 55 wa kaunti hiyo walipiga kura ya kupitisha hoja hiyo kuletwa bungeni ili kujadiliwa na kupigiwa kura.

Wanamlaumu gavana Kidero(ODM) kwa utepetevu na utumizi mbaya wa mamlaka pamoja na ufisadi.

Awali zoezi hilo nusura litibuke pale wajumbe hao walipozua vurugu baada ya spika wa bunge hilo Ole Magelo kumwagiza mwakilishi wa Eastleig kusini Nelson Masika(CORD) kuondoka bungeni kwa kukiuka kanuni.

Hata hivyo hatua hiyo haikupokelewa vyema na baadhi ya wajumbe hao ambao walianza kuvutana mashati na maafisa wa maadili waliofika kumtoa nje kwa lazima.

Wiki jana zoezi hilo lilikwama baada ya wawakilishi hao kuzua vurugu bungeni humo na kupigana.

Iwapo bunge hilo litapiga kura ya kutokuwa na imani na Kidero, jina lake litapelekwa kwa bunge la seneti kwa mjadala zaidi.

Aidha  gavana huyo pia atapewa zamu ya kufika mbele ya bunge hilo ili  kujitetea.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES