Mwanaume mmoja apewa Onyo la mwisho kumkamata jogoo mpiga kelele la...

Mwanaume mmoja apewa Onyo la mwisho kumkamata jogoo mpiga kelele la sivyo atachukuliwa hatua

by -
0 388

Mwanaumme mmoja katika mji wa Pittsburg inchi marekani amepewa siku 30 kumkamata jogoo mpiga kelele la sivyo korti itamchukulia hatua.

Mwanaume huyo aliamuriwa kumkamata jogoo huyo anayeaminika kuishi kwake na ambaye amekuwa akiwapigia majirani wake makelele kila anapowika.Majirani kadhaa wake Gaston waliwasilisha malalamishi kortini wakisema kuwa jogoo huyo alikuwa akiwapigia kelele na kesi hiyo imekuwa ikiendelea tangu mwezi Julai.

Mwanaume huyo kwa jina la Henry Gaston aliambia mahakama kuwa Jogoo huyo si wake na amejaribu kumkamata jogoo kwa namna zote ziwezekanavyo zikiwemo kuhusisha idara ya kuwakamata wanyama lakini hajafua dafu.

Gaston aliambia mahakama kuwa alikuwa amejaribu kumuua jogoo huyo kwa kuumpa sumu ya panya lakini jogoo huyo anayeaminika kuwa mjanja aliweza kuepuka sumu hiyo.

Jirani mwingine Sharon Hudges aliyekuwa amekamatwa kwa kushukiwa kuwa mwenye jogoo huyo hapo awali alikuwa ameomba mahakama msamaha na kusema kuwa aliamini hakuna anayeweza kumkamata jogoo huyo kama idara ya kuwakamata wanyama ilikuwa imeshindwa .

Hakimu alimshauri Gaston kumkamata jogoo huyo kwa kumwekea mtego wa wavu.
Jogoo haziruhusiwi katika mji huo.

Comments

comments