Mjane wa mhubiri mwingine wa kiislamu akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

Mjane wa mhubiri mwingine wa kiislamu akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

by -
0 346

Mombasa, KENYA:Mjane wa mhubiri Samir Khan amekamatwa na maafisa wa polisi huko Tiwi kaunti ya Kwale.

Samira Yakub Khan alikamatwa jumatatu baada ya kuwekewa mtego ambapo alielezwa aelekee kwa ofisi ya chifu kuchukua mzigo wake kabla ya kukamatwa na maafisa waliovalia kiraia.

Mkuu wa polisi huko Msambweni Benjamin Rotich alisema mshukiwa anahusishwa na visa vya ugaidi huko Kilifi na pia uvamizi katika kituo cha polisi cha Central mnamo septemba tarehe 11.

Wakati huo huo Mjane wa marehemu sheikh Aboud Rogo pamoja na wasichana watatu wanaohusishwa na uvamizi wa kituo hicho cha polisi cha Central hapa Mombasa, walishtakiwa kwa pamoja katika mahakama ya Shanzu.

Wanadaiwa kuwafahamu washukiwa wa kigaidi waliovamia kituo hicho.

Lakini wote walikana mashtaka hayo.

Comments

comments