Seneta wa Nairobi Mike Sonko afika mahakamani Mombasa

Seneta wa Nairobi Mike Sonko afika mahakamani Mombasa

by -
0 647

Mombasa:KENYA:Mahakama ya Mombasa imempa muda wa miezi 2 seneta wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko kueleza aliko mwenyekiti wa kundi la Mombasa republican council-MRC Omar Mwamnuadzi.

Hii ni baada ya Sonko kufika mahakamani siku ya ijumaa kufuatia agizo la awali la mahakama kumtaka aelezee aliko Mwamnuadzi aliyekosa zaidi ya vikao vitatu vya kesi inayomkabili.

Sonko hata hivyo alisema hakufahamu ikiwa mwenyekiti huyo wa MRC alikuwa akikosa vikao vya kesi dhidi yake hadi alipopokea agizo la kumtaka afike mahakamani.

Alisema awali alifahamishwa tu kuwa Mwamnuadzi alikuwa na matatizo ya kiafya.

Mahakama ya Mombasa mwishoni mwa mwezi jana ilimtaka Sonko afike mahakamani kuelezea aliko Mwamnuadzi kwani ndiye aliyemsimamia dhamana iliyomuachilia kutoka kizimbani alipozuiliwa kwa madai ya kuandaa mikutano bila idhini.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES