Wanahabari waandamana kutaka kazi yao iheshimiwe

Wanahabari waandamana kutaka kazi yao iheshimiwe

by -
0 554
Waandishi wa habari wakiandamana katika barabara ya Moi mjini Mombasa

Mombasa, KENYA: Waandishi wa habari mjini Mombasa wamepanga maandamano ya amani kulalamikia ongezeko la visa vya waandishi wa habari kukandamizwa wakiwa kazini.

 Wanahabari wanasema baadhi yao wamekuwa wakishambuliwa na hata wengine kufariki katika hali ya kutatanisha huku visa hivyo vikionekana kana kwamba vimechochewa na watu fulani walio na ushawishi.

Maandamano yalianza Jumatano asubuhi katika bustani ya Uhuru iliyo barabara ya Moi mjini Mombasa.

Waandishi hao wa habari wamepanga kuandamana hadi ofisi za wakuu wa idara ya usalama kuwasilisha malalamishi yao.

Wanapitisha ujumbe katika mitandao ya kijamii hasa twitter wakitumia kitambulisha mada yaani hashtag #JournalistsUnderSiege

Tangu mwaka wa 1999, waandishi wapatao 9 wamefariki katika hali isiyoeleweka na wanahabari wanasema hakujawahi kutolewa ripoti zifaazo za uchunguzi huku kifo cha karibuni kikiwa cha mwandishi wa kampuni ya Standard Group aliyefariki mapema mwezi huu nyumbani kwake Kilifi katika hali iliyoibua maswali.

Wanahabari mjini Nairobi nao pia waliandamana mapema mwezi huu kutaka kazi yao iheshimiwe na baadaye kuwasilisha kilio chao kwa maafisa wakuu wa usalama mjini humo.

Wamechukua hatua hiyo huku wakikosoa baadhi ya vyombo vya kutetea maslahi ya wanahabari wakisema havijawajibikia majukumu yao .

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES