Genge la majambazi lavamia na kujeruhi wakaazi Likoni

Genge la majambazi lavamia na kujeruhi wakaazi Likoni

by -
0 393

Mombasa, KENYA: Watu wanne wanauguza majeraha waliyoyapata walipovamiwa na genge la watu wanaotajwa kuwa majambazi eneo la Likoni karibu na msikiti bilal usiku wa kuamkia Jumatatu.

Kulingana na polisi, genge hilo la watu wasiojulikana lilijihami kwa mapanga na visu walivyotumia kuvamia na kuwajeruhi wakaazi kabla ya kuwaibia mali yao.

Imeripotiwa lilikuwa la watu wasiopungua  20.

Wakaazi wa eneo hilo wanaripotiwa kuingia wasiwasi kufuatia tukio hilo la usiku wa kuamkia Jumanne.

Polisi wanasema wanachunguza kubaini lengo la kundi hilo na ikiwa limeshawishiwa kisiasa.

Majeruhi wamelazwa katika hospitali tofauti mjini Mombasa.

Comments

comments