Binti ashtakiwa kwa kujaribu kumtupa mtoto ndani ya kisima

Binti ashtakiwa kwa kujaribu kumtupa mtoto ndani ya kisima

by -
0 340

Mombasa,KENYA:Mahakama ya Mombasa imeambiwa kuwa msichana anayekabiliwa na shtaka la kujaribu kurusha mtoto ndani ya kisimani cha maji, alitaka kufanya hivyo kwa kuwa alikataliwa na babake.

Biberone Umazi ambaye ni afisa wa polisi wa kituo cha polisi cha Makupa aliambia mahakama kuwa mshukiwa aliagizwa na babake mtoto atoe mimba kabla ya kujifungua.

Umazi alisema baada ya kufanya mahojiano na mshukiwa, alifahamu kuwa babake mtoto alisisitiza kutomsaidia msichana huyo baada ya kupuuza agizo la kutoa mimba hiyo.

Shahidi mwingine ambaye ni jirani ya mshukiwa aleeleza mahakama kuwa mshukiwa alikuwa mlevi wakati wa jaribio hilo.

Santal Samir Matano anadaiwa kujaribu kutupa mtoto wa siku saba katika kisima cha maji mwezi Julai katika eneo la Moroto Tudor hapa Mombasa.

Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi tarehe 22 iwapo mshukiwa anakesi ya kujibu.

Mhariri: George Otieno

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES