Mkewe Aboud Rogo kuzuiliwa rumande kwa siku 7

Mkewe Aboud Rogo kuzuiliwa rumande kwa siku 7

by -
0 523

Mombasa,KENYA:Mahakama ya mombasa imeagiza mjane wa Sheikh Aboud Rogo azuiliwe kwa siku 7 ili kuwezesha uchunguzi kukamilika.

Hapo jana mjane huyo Haniya Said Sagaar alikosa kufunguliwa mashtaka baada ya kiongozi wa mashtaka kuiomba mahakama iruhusu aendelee kuzuiliwa.

Upande wa mashtaka uliwasilisha ombi katika mahakama kutaka azuiliwe kwa siku 14 kuwezesha uchunguzi kukamilika.

Haniya Said Sagaar anahusishwa na shambulio lilillotokea katika kituo cha polisi cha Central jumapili iliyopita.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 23 mwezi huu.

Mhubiri huyo aliuawa mwaka 2012 katika barabara ya Mombasa-Malindi karibu na kituo cha polisi cha Bamburi.

Comments

comments