Shule za Lamu bado zimefungwa miaka miwili baadae

Shule za Lamu bado zimefungwa miaka miwili baadae

by -
0 293

Lamu,KENYA:Shule nne za msingi zilizofunguwa katika wadi ya Basuba kaunti ya Lamu bado hazijafunguliwa miaka miwili baadae.

Hii ni licha ya shule zote za umma kufunguliwa kote nchini kwa muhula wa tatu majuma kadha yaliyopita.

Shule za Basuba, Mangai, Milimani na Mararani zilifungwa kufuatia visa vya uvamizi wa magaidi wa Al-Shabaab vilivyokuwa vikishuhudiwa mara kwa mara eneo hilo.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa shule zote nne bado zimebakia mahame.

Baadhi ya wazazi waliohojiwa na Baraka FM huko Basuba wanasema walimu waliokuwa wakihudumu shuleni humo walitoroka na kurudi makwao.

Wameitaka serikali kubuni mikakati kabambe itakayohakikisha shule za Basuba zinafunguliwa

Comments

comments