Baba wa wasichana waliouawa kwa kushambulia kituo cha polisi ahojiwa

Baba wa wasichana waliouawa kwa kushambulia kituo cha polisi ahojiwa

by -
0 592

Mombasa,KENYA:Baba wa wasichana wawili waliouawa waliposhambulia kituo cha polisi cha Central hapa Mombasa siku ya jumapili anahojiwa.

Duru za kuaminika zinasema kuwa mzee huyo alihojiwa na maafisa wa kitengo cha kukabili ugaidi nchini ATPU katika kituo cha polisi cha Urban.

Wasichana hao waliuawa kwa risasi baada ya kuvamia kituo cha polisi wakidaiwa kujihami kwa visu na bomu la petrol.

Maafisa wawili wa polisi waliripotiwa kujeruhiwa kwa kudungwa kisu na washambulizi hao.

Hayo yakijiri idara ya usalama hapa Mombasa inasema imemkamata mshukiwa wa 4 anayehusishwa na kisha hicho cha uvamizi wa kituo cha polisi kwa lengo la kutekeleza shambulizi la kigaidi.

Inadaiwa mshukiwa huyo ambaye ni mwanamume alikamatwa baada ya ripoti kuibuka kuwa awali alikuwa ameonekana akiwa na washukiwa waliouawa.

Wengine watatu waliwakamatwa na polisi na wanasaidia katika uchunguzi.

Katika kisa hicho, wanawake watatu waliuawa na polisi walipojaribu kushambulia maafisa wa polisi waliokuwa katika eneo la mapokezi katika kituo hicho cha polisi.

Taarifa zaidi na Joseph Jira na Weldon Kemboi

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES