Mlalamishi ataka kesi dhidi ya MCA wa Shanzu iondolewe akidai kutishiwa maisha.

Mlalamishi ataka kesi dhidi ya MCA wa Shanzu iondolewe akidai kutishiwa maisha.

by -
0 469
Mwakilishi wa wadi ya Shanzu Maimuma Mwasasi

Mfanyabiashara wa hapa Mombasa amewasilisha ombi katika mahakama ya Mombasa kutaka kuondoa kesi ya ufisadi inayomkabili mwakilishi wa wadi ya Shanzu.

Layer Mourine Aketch ambaye ni mlalamishi katika kesi hiyo ameambia mahakama kuwa kesi hiyo imemsababishia kutishiwa maisha kupitia kupigiwa simu na pia jumbe za simu.

Layer pia ameambia mahakama kuwa aliandikisha taarifa tatu zaidi kuhusu kesi hiyo katika tume ya kukabiliana na ufisadi nchini lakini anahisi tume hiyo ina njama ya kutaka kesi hiyo isiendelee na hata kutomhusisha.

Aketch ameelezea mahakama kuwa aliripoti visa vya kutishiwa maisha zaidi ya mara tatu katika kituo cha polisi cha Bamburi na mtwapa lakini hatua yoyote haikuchukuliwa.

Kiongozi wa mashtaka eugine wangila amepinga ombi la kutaka kesi hiyo iondolewa na kutaka mahakama iwape muda wa kuwawezesha kufanya uchunguzi dhidi ya madai ya mlalamishi kabla ya kesi kuendelea.

Wangila pia amesema kuwa tume ya kukabiliana na ufisadi inahusika katika kesi zingine na kuripotiwa visa vya ufisadi dhidi ya tume hiyo ni jambo lilalohitaji uchunguzi zaidi.

Hakimu Teresia   Matheka amesema mahakama itatoa uamuzi dhidi ya s ombi la mlalamishi tarehe 30 mwezi huu.

Mwakilishi wa  wadi ya shanzu Maimuna Mwasasi pamoja na Christopher Karisa wanakabiliwa na shtaka la kupokea shilingi laki tano kutoka kwa Mourine Aketch kwa madai wangemsaidia kusuluhisha mzozo   wa shamba dhidi yake na serkali ya kaunti.

Comments

comments