Bunge la seneti launda kamati ya watu 11 kuchunguza hatma ya gavana...

Bunge la seneti launda kamati ya watu 11 kuchunguza hatma ya gavana Gachagua

by -
0 327

Nairobi,KENYA:Bunge la Seneti limeunda kamati ya maseneta 11 kuchunguza hatua ya bunge la kaunti ya Nyeri kumtimua mamlakani gavana wa Nyeri Nderitu Gachagua.

Wabunge 32 kati ya 45 wa kaunti ya Nyeri walipiga kura ya kutokua na imani na gavana Gachagua kwa madai ya ufisadi na utumiaji mbaya wa mamlaka.

Kamati hiyo ya seneti sasa ina siku 10 kuchunguza iwapo madai hayo ni ya kweli na kuwasilisha ripoti yao.

Muungano wa CORD umepata nafasi tano katika kamati hiyo huku Jubilee ikipata nafasi sita.

Wanachama wa kamati hiyo ni pamoja na maseneta Lenny Kivuti (Embu), Peter Mositet (Kajiado), Kimani Wamatangi (Kiambu), Billow Kerrow (Mandera), Isaac Melly (Uasin Gishu), Joy Gwendo (seneta mteule) kutoka muungano wa Jubilee.

Wengine ni George Khaniri (Vihiga), Stewart Madzayo (Kilifi), Judith Achieng Sijeny (seneta mteule), Moses Kajwang (Homa Bay) na Janet Ong’era (seneta mteule) wa CORD.

Katika hotuba yake kwa bunge hilo, kiongozi wa wengi Kithure Kindiki, aliwaomba maseneta hao kuharakisha kuskiliza hoja hiyo ili watu wa Nyeri wasikose mwakilishi.

Naye kiongozi wa wachache Moses Wetangula, aliwaonya wawakilishi wa wadi wa Nyeri dhidi ya kulishurutisha bunge hilo la seneti kukubaliana na hatua yao bila ya kuwepo utaratibu wa uchunguzi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES