Gavana wa Nyeri Nderitu Gachagua atimuliwa ofisini

Gavana wa Nyeri Nderitu Gachagua atimuliwa ofisini

by -
0 413

Nyeri, KENYA: Wawakilishi wa kaunti ya Nyeri wamepitisha hoja ya kumwondoa ofisini gavana -Nderitu Gachagua.

Gachagua ameondolewa kufuatia madai ya ufisadi na utumizi m-baya wa mamlaka.

Takriban wabunge 32 kati ya 46 wa bunge la kaunti hiyo walipiga kura ya kumtimua gavana huyo.

Hoja ya kumwondoa gavana huyo iliwasilishwa bungeni na mjumbe wa wadi ya Kiganjo – Baragu Mutahi.

Awali wabunge hao wa kaunti walikesha ndani ya majengo ya bunge hayo wakisubiri siku mpya kupiga kura kuamua hatma ya Gachagua.

Gachagua ambaye alichaguliwa mwaka 2013, amekua akiugua kwa muda sasa ambapo amekua akisafiri nje ya nchi kwa matibabu ya kiafya.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES