Wanachama wawili wa MRC wahukumiwa kifo

Wanachama wawili wa MRC wahukumiwa kifo

by -
0 498
Mombasa Law courts.

Mombasa, KENYA:Mahakama ya Mombasa imewahakumu kifo wanachama wawili wa kundi la Mombasa Republican Council-MRC baada ya kuwakuta na hatia ya kuwaua maafisa wanne wa polisi mwaka 2013.

Jabiri Ali Dzuya na Bwana Mkuu Alwani walipatikana na hatia ya kuwaua maafisa ya polisi akiwepo Atieno Owour, Salim Kimutai, Stephen Maithya na Andrew Songira usiku wa kuamkia uchanguzi mkuu wa mwaka 2013.

Akitoka hukumu hiyo jaji Martin Muya alisema kutokana na ushahidi kortini, Dzuya alikuwa mwenyekiti wa kundi la MRC na walikuwa na nia ya kutatiza uchanguzi huo.

Hata hivyo mahakama iliwaachilia washukiwa wengine wawili kwa ukosefu wa ushahidi wa kutosha.

Kundi la MRC limekuwa likishinikiza ukanda wa pwani kujitenga na serikali ya Kenya na kujitawala kivyake.
Wafuasi wa kundi hilo wamekuwa wakiendeleza wito wa “pwani si Kenya”.

Wakili wa washukiwa Fred Langat alisema atakata rufaa.

Imehaririwa na Joseph Jira

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES