Washukiwa wa ugaidi wauawa Mombasa

Washukiwa wa ugaidi wauawa Mombasa

by -
0 477

Mombasa,KENYA: Polisi wanasema wamewauwa washukiwa wawili wa kundi la kigaidi la Al-shabaab  katika mtaa wa Tudor estate-Mshomoroni hapa Mombasa.

Polisi inasema mmoja wa washukiwa ametoroka na majeraha ya risasi.

Wanasema wamenasa risasi 17, vilipuzi vitatu na maguruneti 3 kutoka kwa washukiwa hao.

Wamewatambua kama Salim Omar na Salim Abdalla.

Ocpd wa Kisauni Walter Abondo amesema washukiwa wamehusika na visa kadhaa vya ugaidi na wamekuwa wakisakwa na vyombo vya usalama.

Wanamsaka aliyetoroka na majeraha ya risasi.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES