Mfanyabiashara apigwa risasi na pesa kuibwa Likoni-Mombasa

Mfanyabiashara apigwa risasi na pesa kuibwa Likoni-Mombasa

by -
0 466

Mombasa, KENYA:Washukiwa wa ujambazi wanasemekana wamempiga risasi mfanya biashara mmoja na kutoweka na kitita cha shilingi laki mbili baada ya kuvamia maduka matatu ya m-pesa eneo la likoni mjini Mombasa.

Mfanyabiashara aliyepigwa risasi alitambuliwa kama Kelvin Ndunda.

Washukiwa hao watatu waliokuwa kwa pikipiki walitekeleza wizi huo saa chache baada ya kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohammed Maalim, kuongoza mkutano wa usalama katika eneo la Ijara likoni.

Hiki ni kisa cha nne katika kipindi cha wiki mbili sasa.

Polisi wanaamini bunduki inayotumwa na washukiwa ni ile iliyoibwa kutoka kituo cha polisi cha Likoni.
Kwa sasa wanawasaka washukiwa wa wizi huo.

Comments

comments

SIMILAR ARTICLES