Mtu anayehusishwa na mauaji akamatwa kwa kuhepa mahakama

Mtu anayehusishwa na mauaji akamatwa kwa kuhepa mahakama

by -
0 361

Mombasa,KENYA:Mahakama kuu ya Mombasa imetoa kibali cha kukamatwa kwa mwanamume anayedaiwa kumwua mpenzi wake wa kike baada ya kukosa kufika mahakamani kufuatia agizo la mahakama.

Joseph Kamau Nyambura anadaiwa kumua Lavina Muya mwaka wa 2011 katika eneo la Likoni hapa Mombasa.

Awali mshukiwa alikuwa ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano baada ya kukana shtaka hilo la mauaji.

Wakati huo huo Mwanamume mmoja ameshtakiwa katika mahakama ya shanzu kwa madai ya kumteka nyara mtoto.

Kennedy Ogora Francis anadaiwa kumteka nyara mtoto huyo tarehe 16 mwezi huu katika eneo la Mishomoroni Kisauni hapa Mombasa.

Pia anakabiliwa na shtaka la kuitisha shilingi elfu 25 kutoka kwa mzazi wa mtoto huyo na kutishia kumjeruhi iwapo hatapewa pesa hizo.

Mshukiwa alikubali mashtaka na sasa anasubiri huku.

Comments

comments